Tunafanya kazi ya kubadilishamazingira na dunia yetu!
Drömmarnas Hus tunafurahi kutumia utamaduni, asili ya ubunifu wa kujifunza na uwezo wakutengeneza zana ya mabadaliko ya jamii.
Tangu 1990 tupo Rosengård, Malmö. Mwaka 2000 tulibadilisha jina letu kutoka Teater X, nakuitwa Drömmarnas Hus. Sisi ni shirika lisiyo na faida.
Mradi wa mwisho tulioufanya ulihusisha maelfu ya watoto na vijana ambao waliweza kuwasiliana na waatalamu wa mambo yanayohusiana na jamii na utamaduni. Tunafanya kazi wakati wa shule na pia tunakaribisha mawasiliano baada ya shule, na huduma zote ni bure.
Tuna ofisi yetu Rosengård lakini tunafanya kazi mkoa wote wa Skåne, pia tuna mawasiliano na mashirika mengine yanayofanya shughuli kama zetu Ulaya nzima. Dhumuni la shirika letu nikusaidia watu wa mataifa mbalimbali kuweza kuishi pamoja nakuweza kufanikisha mahitaji ya vijana kumuwezesha kuishi katika misingi ya maadili mema.